RAIS
Jakaya Kikwete amesema kampuni nyingi nchini zimeshindwa kuendelea
kutokana na kuendeshwa kifamilia, badala ya kuuza hisa na kumilikiwa na
umma. Akizindua Karakana ya Ndege ya Kampuni ya Precision Air jana,
Rais Kikwete alisema kampuni nyingi nchini zinatakiwa kubadili mfumo wa
uendeshaji.
“Watanzania
wanaimiliki Precision Air kwa asilimia 59, huu ni mfano wa kuigwa kwa
sababu ziko kampuni nyingi zimebaki kuwa za familia tu,” alisema
Kikwete. Hata hivyo, Rais Kikwete alisema suala la hisa kwenye sekta ya
anga bado ni biashara ambayo watu wengi hawajaielewa vizuri tofauti na
sekta zingine kama benki. Alipongeza shirika hilo kwa kutengeneza
karakana hiyo na kuitaka iwe na viwango vya hali ya juu vitakavyokidhi
matakwa ya kimataifa.
“Tuache
viwango vya kibongobongo, tukilipua tutahatarisha ustawi wa ndege na
kampuni zitakazokuwa zinatumia karakana hii,”alisema. Pia, alitaka
Wizara ya Uchukuzi na ile ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kujenga chuo cha
ufundi wa ndege nchini.
“Siku
hizi sijui hata wanajifunzia wapi... tunaona wanaruka tu
walikojifunzia wanajua wenyewe,”alisema Rais Kikwete. Naye Mwenyekiti
wa Bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo, Michael Shirima alisema hadi
sasa wana mtaji wa dola 2 milioni za Marekani na kwamba, wana ndege 12
huku wakimiliki tisa kati ya hizo.
No comments:
Post a Comment