Monalisa mtayarishaji na mwigizaji bora wa filamu Swahiliwood.
MWANADADA mahiri katika uigizaji
tasnia ya filamu Swahiliwood Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ amesema kuwa
anatumia muda mwingi kusoma soko la filamu na kupunguza kushiriki
filamu kila mara jambo ambalo linamfanya aendelee kuwa bora kwa kipindi
chote kwani wakati wasanii wengine wakishiriki filamu nyingi kwa mwaka
lakini yeye ni agharabu kuigiza hata filamu tano kwa mwaka.
Monalisa mwigizaji asiye na makeke Swahiliwood.“Mara nyingi sipendi kuwa Location (Sehemu ya kurekodia) kila wakati kwa kufanya hivyo naamini inaweza kuwa ni sehemu ya kupoteza umakini na ubora wa kazi yenyewe lakini kama ukiigiza filamu chache lazima uendelee kufanya vizuri kuna wakati nakaa hata mwaka kwa kurekodi filamu moja tu, pia kwa sasa napenda kuigiza filamu zangu ili kulinda sanaa yangu,”anasema Monalisa.
Monalisa ndio msanii wa kike wa kwanza kuigiza filamu iliyotikisa na kuleta changamoto kwa watengenezaji wa filamu Swahiliwood baada ya kushiriki filamu ya Girlfriend na wasanii wa muziki wa kizazi kipya mwaka 2003, Monalisa ameweza kushinda tuzo kadhaa akiwa ni mwigizaji bora wa kike baadhi ya tuzo ni ZIFF, Bora za 2010, lakini pia ndio msanii wa kike aliyeweza kutuza muonekano wake kwa muda mrefu huku mashabiki wakimwita Angelina Jolie wa Bongo
No comments:
Post a Comment