Saturday, 7 July 2012
Jason Derulo kutua rwanda
Imethibitika kwamba staa wa ngoma ya Watcha Say, iliyotoka mwaka 2009,
na kuvuma mwaka jana hapa nchini, jason derulo ndio atakuwa mtumbuizaji
mkubwa kwenye fainali za shindano kubwa la muziki nchini Rwanda,
lijulikanalo kwa jina la Primus Guma Guma Superstar ambalo linafanyika
kwa mara ya pili nchini humo.Habari za uhakika zinasema kwamba
Derulo kwa kushirikiana na wasanii wakubwa wa rwanda, watapanda jukwaa
moja tarehe 29 ya mwezi huu, huku yeye akiwa kama mtumbuizaji, na
wasanii wa Rwanda wakichuana ili kumpata staa mkubwa wa ukweli kutoka
nchini humo, miongoni mwa wale wanaowika.Mwaka jana, shindano hilo lilifanyika na mwanamuziki wa R&B nchini humo Tom Close, aliibuka mshindi.Tofauti
ya shindano hili na mashindano kama BSS na Tusker Project Fame, ni
kwamba lenyewe hushindanisha wasanii waliofanikiwa tayari na wasanii
kumi pekee ndio huchaguliwa kushiriki, kama ilivyokuwa kwa Mfalme wa
Rhymes Tanzania.Wasanii hao hutumia nyimbo zao wenyewe wakati wa shindano hilo.Vigezo
vya wanamuziki kushindana kwenye shindano hilo ni lazima awe na miaka
18 na kuendelea, awe na wimbo uliohit na awe anafanyia muziki nchini
Rwanda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment