TAARIFA KWA UMMA
Baraza
la Madaktari Tanganyika limepokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba, baadhi ya Madaktari waliopata
usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship),
waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kati ya tarehe 23 na 29 mwezi Juni
2012. Madaktari hao walipangiwa kutoa huduma kwa wagonjwa katika
hospitali za Muhimbili, K.C.M.C, Rufaa Mbeya, Bugando, Amana, Temeke,St.
Francis- Ifakara, Mwananyamala, Sekou Toure, Haydom na Dodoma.
Kufuatia mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua
iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo kuripoti kwa Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Katika
hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
aliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la Madaktari Tanganyika kwamba,
Madaktari waliogoma walikataa kutoa huduma za kitaalamu, ikiwa ni wajibu
wao, na kwamba kitendo hicho kilihatarisha maisha ya wagonjwa katika
hospitali husika na pia ni kinyume na maadili ya taaluma ya udaktari.
Kufuatia
malalamiko hayo, Msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika,
alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la Kufanya
Uchunguzi (Preliminary Examination) dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baraza
la Madaktari Tanganyika limebaini kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha
15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, Madaktari waliokuwa kwenye
mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa
wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa
muda (Provisional Registration).
No comments:
Post a Comment