Hivi
karibuni Benki hiyo ilitunukiwa Tuzo ya Dhahabu iliyotolewa na jijini
Geneva Uswis, tuzo hiyo inajulikana kama Century International Gold
Award (ERA).
Lengo
la tuzo hiyo ni kutambua ubora wa huduma zitolewazo kwa wananchi na
taassisi au kampuni mbalimbali lengo lokiwa ni kuhamasisha utolewaji wa
huduma bora kwa wateja.
Mtendaji
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Hussein Mbululo amesema kwamba Benki
yake ilikuwa miongoni mwa Benki 100 zilizoshinda katika tuzo hizo
kutoka nchi 47, tuzo hizo ziligawanywa katika makundi saba.
Amesema kujituma miongoni mwa wafanyakazi katika kuwahudumia wateja pamoja na ubunifu ndio siri kubwa ya mafanikio.
Twiga Bancorp ni Benki inayo milikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%).
Afisa Mtendaji wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akiwa na baadhi ya maofisa wa BID mjini geneva kabla ya kuanza utoaji Tuzo.
CEO wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akisalimiana na Rais na CEO wa BID, Jose Priento mjini Geneva-Uswisi
No comments:
Post a Comment