Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye leo jioni alikwenda
Muhimbili kwa nia ya kumjulia halia, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari
Tanzania, Dk. Stevene Ulimboka, amezuiwa kumuona.Profesa Lipumba, ambaye alikuwa na nia nzuri ya kumjulia hali daktari
huyo, alizuiwa na madaktari wenzie kwa madai kwamba hawamruhusu mtu
yeyote kwani Dk. Ulimboka alikuwa anaendelea na matibabu ndani ya
chumba cha wagonjwa mahututi ICU.Alipofika hospitalini hapo, kwanza alikwenda kwa Meneja Uhusiano wa
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Jumaa Almas ambaye pia
alimueleza hivyo. Profesa Lipumba ni kiongozi wa kwanza wa kisiasa
kwenda Muhimbili kutaka kumjulia hali Dk. Ulimboka.
DK Ulimboka akiwa katika chumba hicho cha icu
No comments:
Post a Comment