..

..
.

Saturday, 16 June 2012

PAMOJA NA AGIZO LA SERIKALI HUDUMA YA JIWE INA PATIKANA HAPA

Mama Mjasiliamali, akiponda kokoto kwa katika eneo la Bonde la Tegeta, mahala ambapo Serikali ilipiga marufuku zoezi la kuendele kuchimba Mawe na Kokoto,  Mama huyu huponda Kokoto na kulipwa ujira na bosi wake kulingana na kiasi alichoponda kwa siku, jambo ambalo linawafanya wenye maeneo haya kuendelea na zoezi hilo kama kawaida. Na sasa watu walio na maeneo mahala hapa wamekuwa wakiuza maeneo ya Viwanja kwa wananchi, ambao baadhi yao wameshuhudiwa na mtandao huu wakiendelea na ujenzi wa nyumba mahala hapa. Je wahusika mpo?? au mnasubiri wakianza kuishi ndiyo muanze kuwatimua??
 Baadhi ya wenye maeneo ya Mawe, wakiendelea kuchimba mawe, mahala hapa.....................

No comments:

Post a Comment

KARIBU