KATIKA hali
ya kujiimarisha kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu, klabu ya Yanga imepanga
kuivamia kambi ya Simba na kusajili wachezaji watatu wa kikosi cha
kwanza cha mabingwa hao wapya wa Bara.
Kwa
mujibu wa taarifa za ndani za Kamati ya Usajili ya klabu hiyo
zilizopatikana jana, zimewataja wachezaji hao kuwa ni beki wa kati,
Juma Nyoso, Juma Jabu na kiungo chipukizi Uhuru Selemani.
Habari
zaidi zinadai kuwa, Wanajangwani wako tayari kumwaga kiasi kikubwa cha
pesa ili kuwanasa nyota hayo walioiwezesha Simba kutwaa ubingwa msimu
huu kabla ya ligi kumalizika.
Mtoa
habari amepasha kuwa, tayari mazungumzo ya awali yamefanyika na
kinachosubiriwa ni uamuzi wa wachezaji hao kukubali ofa na kisha
kusaini mikataba.
“Tumeshafanya
mazungumzo ya awali, kwa sasa hatuwezi kuweka wazi kila kitu lakini
tunachosubiri ni wao kukubali kusaini mikataba kwa ajili ya msimu
ujao," alisema mtoa habari ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini
kwa vile siyo msemaji.
"Tunaamini kama tutawapata, basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika usajili kwa ajili ya msimu ujao," alisema zaidi.
Aidha,
alisema mbali na wachezaji hao pia wana mpango wa kusajili wachezaji
wawili wa kimataifa kutoka Rwanda waliong'ara wakati wa michuano ya
Kombe la Chalenji mwaka jana.
Wachezaji hao ambao ni 'mapacha' wa ushambuliaji wa klabu ya APR ni Meddie Kegere na Olivier Karekezi.
"Kwa sasa hatuna tena tatizo na pesa za usajili, tuna kila uwezo wa kumsajili mchezaji tutakayemtaka," alisema mtoa habari.
"Kwa sasa hatuna tena tatizo na pesa za usajili, tuna kila uwezo wa kumsajili mchezaji tutakayemtaka," alisema mtoa habari.
Juhudi
za kuwatafuta wachezaji hao kuthibitisha madai ya Yanga zilishindikana
isipokuwa mchezaji Uhuru aliyesema: "Nachoangalia ni maslahi niko
tayari kwenda timu yoyote itakayonihitaji na kufika dau."
Aidha,
alisema anashangaa uongozi wa Simba kuwa kimya bila kusema lolote
mpaka sasa wakati wanafahamu mkataba wake umefika tamati.
"Sina
mkataba na Simba kwa sasa na sijaona jitihada zozote za viongozi wala
sijapigiwa simu kufahamishwa kama nitaendelea kubaki ama naondoka. Niko
huru naangalia atakayekuja na dau kubwa," alisema.
Uhuru ameichezea Simba karibu misimu mitatu.
Uhuru ameichezea Simba karibu misimu mitatu.
No comments:
Post a Comment