Riadha Kenya (AK), chombo kinachoshughulika na riadha nchini,
kinapanga kuandaa mfululizo wa mashindano ya mbio ndefu mapema mwaka
ujao ili kuibua vipaji vilivyojificha katika Mkoa wa Kaskazini
Mashariki.
Mwenyekiti wa AK Isaiah Kiplagat alisema hii ni mara ya kwanza kwa
tukio kubwa la riadha kama hili kuanzishwa mkoani. Alisema AK inataka
kuinua mwamko wa riadha katika mkoa na inatumai kuwa baadhi ya
wanariadha wa juu watakuja kukuza mchezo huo.
Ili kuusaidia mkoa kufikia uwezo wake kamili, AK imewapa mafunzo makocha 15, Kiplagat alisema.
“Tumekuwa tukituma timu za Kenya katika mashindano ya kimataifa,
lakini inavunja moyo kuwa mwaka baada ya mwaka, hakuna yeyote kutoka
mkoa huu anayeshiriki – hata katika mashindano ya kitaifa,” aliiambia
Sabahi
kweli si mchwzo kila kitu kuamua na mazoezi hawa jamaa wanaweza kukimbia karibia nusu nchi
ReplyDelete