Sunday, 27 May 2012
Jeshi la Somalia linajiandaa kuchukua majukumu ya kiusalama kutoka majeshi ya kikanda yaliowekwa sehemu mbalimbali nchini, maafisa wa ulinzi Somalia waliiambia Sabahi.
Abdirashid Ibrahim, mkurugenzi wa utawala wa Wizara ya Ulinzi aliiambia Sabahi kwamba wizara inaandaa mpango wa kuviuganisha vikosi vya kijeshi kama ilivyopendekezwa na tume ya pamoja ya usalama (JSC) nchini Somalia.
Katika mkutano wake wa karibuni mjini Mogadishu, tarehe 9 Mei, tume ya pamoja ya usalama ilitoa wito wa kuviunganisha vikosi vya kijeshi nchini Somalia ili kukabiliana na makundi ya al-Shabaab na al-Qaeda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment