Habari
tunazoendelea kuzipata kutokana na suala la sheikh Ponda kupigwa Risasi
hapo tarehe 10-8-2013 (Jana Jumamosi) zimethibitisha kuwa Sheikh Ponda
bado yuko hai na kwamba anatibiwa Muhimbili.
Taarifa za mtoa habari wetu kutoka
Morogoro zinasema kuwa habari za kwamba sheikh Ponda amekufa si za kweli
na kwamba kilichofanya waislaamu kumficha jana ni hofu kuwa jeshi la
polisi “huenda lingemaliza kazi” kama lingejua aliko.
Vile vile chanzo hicho kinadai kuwa,
lengo la askari lilikuwa kuua kwani baada ya kumpiga risasi sheikh Ponda
na kuanguka chini waliondoka eneo la tukio.
Anahoji; “Kama lengo ni kumkamata basi wangeuchukua mwili wake, na si kweli kwamba waislaamu waliwazuia ama kuwafanyia fujo”
KUTOKA DAR ES SALAAM
Jioni hii huko katika msikiti wa
Mtambani jijini Dar Es Salaam, waislaamu kutoka maeneo mbalimbali ya
jiji wamekusanyika kupewa habari kamili za tukio hilo.
Taarifa za awali zinasema kuwa Sheikh
Ponda yupo hospitalini jijini hapo akitibiwa kihalali kabisa na kwamba
vyombo vya dola vinajua alipo.
Taarifa zaidi kutoka katika mkutano huo zinadai kuwa majeraha ya sheikh Ponda ni makubwa na kwamba bega lake limevunjika vibaya.
Mtandao huu utaendelea kukuletea ukweli wa tukio na yale yanayotokana nayo.
No comments:
Post a Comment