Ndege
ya kukodi ya Tanzanair iliyokuwa na marubani wawili, iliyokuwa ikitokea
Msumbiji kwenda jijini Dar es Salaam, imelazimika kutua kwa kusota kwa
tumbo bila kutoa matairi katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara bila
mawasiliano, baada ya ndege hiyo kukata mawasiliano ya umeme ghafla
wakati ikiwa hewani na kuzimika.
Aidha
imeelezwa kuwa marubani wote wawili waliokuwamo katika ndege hiyo bila
abiria yeyote wote wamesalimika na ndege hiyo imeharibika vibaya huku
Propela zake zote zikiwa zimekunjamana. Marubani hao wameueleza mtandao
huu kwa njia ya simu kuwa waliamua kutua katika uwanja huo kwa dharula
baada ya ndege kushindwa kutoa matairi
No comments:
Post a Comment