Habari za kuamika kutoka kwa vyanzo mbalimbali zinadai kuwa wasanii wa mkoa wa Tanga wamelikataa
wazo la mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe la kufanya wimbo wa
pamoja kama Tanga All Stars kwa madai kuwa mradi huo anaufanya ili
kujinufaisha kisiasa.
Hivi
karibuni Mheshimiwa Zitto alikiri kuutaka urais wa Tanzania wakati wa
mahojiano na kipindi cha Makutano cha Magic FM na watu wengi
wamekichukulia kitendo cha kuwa karibu na wasanii wa Tanzania kama njia
ya ya kujiimarisha kisiasa na kuwashawishi vijana walio wengi nchini.
Mwandishi
wetu ameongea na MwanaFA kwa simu jana (August 17) ambaye amesema
wasanii wa Tanga wana program yao wenyewe iliyopo tangu muda mrefu na
wamewahi hata kufanya show za ndani na nje.
Amesema hawawezi kujiingiza kwenye mradi huo wa Zitto kwakuwa umekaa kisiasa zaidi.
Katika
mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM mwezi uliopita, Zitto alidai
kuwa lengo lake ni kila mkoa kuwa na wimbo wa nyota wenye asili ya
mikoa mbalimbali na baada ya Kigoma mkoa wa pili aliokuwa anafanya nao
mazungumzo ni Tanga ambao tayari wamemtosa.
Wakati
Tanga ikishtukia mchezo huo wenye harufu ya siasa, wasanii wa Morogoro
chini ya Afande Sele tayari wameingia mkenge na wamefanya wimbo wa
Morogoro All Stars.
Morogoro All Stars inaundwa na Afande Sele, Koba, Stamina, Belle9, Samir, Criss Wamaria, Nassa, Oten, Dayna na Zilla!
Chanzo kimoja cha uhakika kimeiambia Blog hii kuwa mradi wa Kigoma All Stars umegharimu mamilioni ya shilingi.
Amedai
kuwa kwenye show ya wasanii hao iliyofanyika mwezi uliopita mkoani
Kigoma kila msanii alilipwa si chini ya shilingi milioni moja.
Aidha
Mheshimiwa Zitto aliwahi kudai kuwa Kigoma All Stars itakuwa kampuni
na inajenga kituo cha kuendeleza vijana wenye vipaji mbalimbali mkoani
Kigoma.
Kufuatia
wasanii wa Morogoro kuja na wimbo wao kama wale wa Kigoma, kumekuwepo
na hisia tofauti juu ya miradi hiyo ya wasanii kujiunga na kutoa nyimbo
za mikoa ambapo wapo wanaosema ni kitu kizuri huku wengi wakidai
inaonesha jinsi watu walivyoishiwa na mawazo mapya.
“Uvivu wa fikra na maisha ya kuiga...wangeweza kufanya kitu kingine kizuri cha kibunifu kuliko ku-kopi na ku-paste...upu********....
No comments:
Post a Comment