amesema hataondoa vipande vya mtalaka wake, Russell Brand, katika mkanda wa video wa maisha yake anaotaka kuuingiza sokoni.
Brand alimtaka Perry kuondoa picha zake katika mkanda huo baada ya kuachana miezi kadhaa iliyopita.
Hata hivyo Perry amemtunishia kifua kwa kusema kuwa hataondoa chochote kwa kuwa alikubali kuwamo tangu mwanzo wakati anaanza kurekodi video hiyo.
Pia alisema kuondoa vipande hivyo kutafuta maana ya mkanda huo ambao unasubiriwa kwa hamu.
Baada ya Perry kugoma kumuondoa Brand katika mkanda huo, mwanamume huyo alitaka aone kilichomo kabla haujauzwa, hata hivyo hilo pia limegonga mwamba kwani Perry amekataa kumwonyesha.
No comments:
Post a Comment