..

..
.
Showing posts with label Na abdullrahmanyusuph kutoka TANGA. Show all posts
Showing posts with label Na abdullrahmanyusuph kutoka TANGA. Show all posts

Thursday, 19 July 2012

 

 

 MMILIKI WA BLOG YA MPEKUZI AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

TUNASIKITIKA KUWAJULISHA MMLIKI WA  WA BLOG YA MPEKUZI 
BW: JOHN BENARD ,AMEFIWA NA MAMA YAKE MZAZI   LEO MAJIRA  YA SAA TANO ASUBUHI .
YEYE   PAMOJA NA KUNDI  ZIMA  LA MPEKUZI  TUPO MSIBANI   KUUNGANA NA NDUGU NA  JAMAA.

TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU  MAHALI  PEMA  PEPONI .  AMINA

Saturday, 7 July 2012

NI HATUA NZURI YA UWEZEKANO WA BINADAMU KWENDA KUISHI, DALILI ZAONYESHA KUNA VIUMBE HAI

WANASAYANSI wa anga kwa muda mrefu wamekuwa wakitafuta  uwezekano wa maisha katika sayari nyingine, mbali na dunia.Kuna imani kuwa kwenye sayari hizo, huenda zikapatikana raslimali nyingi kwa urahisi kuliko duniani ambako binadamu wameishi mamilioni ya miaka  hadi sasa.
Wataalamu hao wa anga wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda sasa na moja ya mambo muhimu wanayoangalia ni upatikanaji wa maji. Popote maji yanapopatikana, wanaamini maisha yanawezekana.Moja ya sayari ambayo wamekuwa wakiichunguza kwa miaka mingi sasa ni Mars, ambayo ni ya nne kutoka kwenye jua. Dunia ni ya tatu.

Sababu kuu za kuichagua sayari hii tofauti na zingine ni kwamba, hali ya hewa inatofautiana kidogo sana na ya dunia.
Sayari nyingine kama Mercury na Venus, zipo karibu zaidi na jua na hali ya joto iko juu kiasi kwamba hali ya maisha inaweza kuwa taabu.


RAISI JAKAYA KIKWETE AUDHURIA SABASABA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi katika viunga vya uwanja wa maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Wananchi walijipanga njiani na kusalimiana naye wakati yeye na Mama Salma Kikwete walipokuwa wakitembelea banda moja hadi lingine.

Monday, 2 July 2012

MADAKTARI MSIPOTEZE MUDA WENU KUGOMA. MAANA SERIKALI HAIWEZI KUWALIPA MILIONI 7 KWA MWEZI...JAKAYA KIKWETE

SEHEMU YA HOTUBA  YA JK

.......Sina budi kusisitiza  kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa.   Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile. Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=.  Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.
Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho.  Nasi tutamtakia kila la heri.  Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo.  Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka.  Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi.  Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24.  Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe.  Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.
  Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma.   Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.

Gari la Waziri wa Habari, Mukangara lililopata ajali na kujeruhi

Hili ndilo gari ambalo alilokuwa akitumia Waziri  wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, na kupata nalo ajali  juzi akiwa safarini kutoka Dodoma kuelekea jijini Mwanza kikazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Antony Luta, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi katika Kata ya Nyandekwa wilayani Igunga mkoani hapo, ikihusisha gari lenye namba za usajiri STK 8780.

Luta alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi la Green Star lenye namba za usajili T939 TRA ambalo lilikuwa likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam, alipokuwa akijaribu kulipita lori katika mlima huku gari la Waziri huyo likitokea upande wa pili.

Dereva wa Waziri aliyetambulika kwa jina la Saidi Komando, alijaribu kulikwepa basi hilo, lakini akashindwa na hivyo gari likapinduka mara tatu na kusababisha watu watatu akiwemo Waziri Fenella, kujeruhiwa.

Kamanda Luta alisema mara baada ya ajali hiyo, Waziri huyo na majeruhi wengine walikimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Nzega kwa matibabu na kwamba mipango ya kuwahamishia katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma zinafanywa.

Dereva wa basi la Green Star, Daniel Chawa (32), alikamatwa baadaye na polisi wilayani Igunga, baada ya kuwa amekimbia awali na hivyo atafikishwa mahakamani.

Hali ya Dkt. Mukangara inaendelea vizuri.

Akiongea na Globu ya Jamii sasa hivi yupo Dar es salaam alikorejea jana jioni na kupata matibabu zaidi katika kitengo cha mifupa cha MOI hospitali ya Muhimbili. Amesema baada ya kuchukuliwa vipimo vyote, ameonakana hana madhara mwilini zaidi ya michubuko na  majeraha mengine madogo. Anashukuru kwamba wote walikuwa wamefunga mikanda na kwamba air-bags za gari hilo zimeokoa maisha yao.

Amewashukuru sana madaktari wa Nzega na wa kitengo cha dharura cha Muhimbili ambao walimhudumia pamoja na wa hospitali ya Regency alikopatiwa vipimo vya CT-Scan. Pia anawashukuru Watanzania wote waliomuombea apate nafuu, wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

Saturday, 30 June 2012

Kugombana Na Madaktari Ni Uchuro - Prof. Mbele

Mgomo wa madaktari umeanza tena, siku chache zilizopita. Inasikitisha kuona kuwa tumefikia hali hiyo. Ukiniuliza nani namhesabu kama mwajibikaji mkuu aliyesababisha tatio hili, nitakuambia kuwa ni serikali ya CCM. Huo umekuwa msimamo wangu tangu pale ulipotokea mgomo wa mwanzo wa madaktari wiki kadha zilizopita. Nilieleza msimamo huo hapa.

Siku chache zilizopita, nilimsikiliza mwenyekiti wa madaktari wanaogoma, Dr.Stephen Ulimboka, akiongelea jinsi uhaba wa vitendea kazi ulivyo. Alitaja mfano wa kifaa cha "CT-scan" ambacho kimeharibika Muhimbili yapata miezi mingi iliyopita.

Kama nilivyosema katika makala yangu ya mwanzo, sera za serikali ya CCM zinasabisha upotevu mkubwa wa mali ya Tanzania, kama vile madini. Serikali yenyewe imekiri kuwa mikataba ya madini ya siku zilizopita ilikuwa ni ya hasara kwa Taifa. Lakini je, serikali imeshamwajibisha yeyote aliyehusika katika kusaini mikataba hiyo?

Je, ni kweli kuwa nchi hii haiwezi kununua hicho kifaa cha "CT-scan"? Kutokana na sera mbovu za CCM, makampuni kama Barrick yanafaidika sana na dhahabu yetu wakati sisi, ukifananisha na mapato wanayopata wao, sana sana tunaambulia mapato duni sawa na njugu kiganjani, na tunaambulia uharibifu wa mazingira na afya za watu wanaoishi maeneo ya migodini,

Kitu kimoja kinachokera katika mgogoro huu baina ya serikali na madaktari ni jinsi madai ya madaktari yanavyopotoshwa. Wako ambao wanaongea kama vile wanachodai madaktari ni posho na maslahi yao tu. Ukweli ni kuwa madaktari wana madai ya msingi ya kuwatetea wananchi. Kuna uchakachuaji wa makusudi unaofanywa kuhusu jambo hilo, ili ionekane kuwa madaktari hawajali maishai ya wananchi.

Ni kweli kuwa mgomo huu unaathiri maisha ya wa-Tanzania. Hili si jambo jema. Lakini serikali haina haki ya kuwashutumu madaktari kwa hoja hii ya kutojali maisha ya wa-Tanzania, wakati serikali hiii hiii inawakumbatia hao wanaoitwa wawekezaji ambao wengi wao wanahujumu maisha na afya za wa-Tanzania, achilia mbali kuharibu mazingira maeneo ya migodini. Serikali ingekuwa haifanyi hayo, ingekuwa na haki ya kuwaandama madaktari kwa hoja hii ya kuathiri maisha ya wa-Tanzania.

Katika mgogoro baina ya serikali na madaktari, kuna pia suala la serikali kutumia mwanya wa sheria na uamuzi wa mahakama. Serikali haifanyi haki inapokwepa kuwajibika kwa yale yanayodaiwa na madaktari, madai ambayo ni ya kweli, na yako katika uwezo wa serikali na nchi yetu hii ambayo ina utajiri mkubwa. Kama suala ni sheria na maamuzi ya mahakama, sote tunakubali kuwa sheria ichukue mkondo wake.

Lakini kinachokera ni kuwa serikali inatumia mwanya huu kufunika kile ambacho sisi wengine tunakiona ni uzembe na kutowajibika kwa serikali yenyewe. Madai ya madaktari ni ya msingi, na yako katika uwezo wa serikali hii. Kwa serikali kutowajibika hapo na kukimbilia mahakamani kuwabana madaktari kwa kipengele cha sheria tu, sio jambo la haki na haliiweki serikali katika sura nzuri, kwa mtazamo wangu.

Kama nilivyosema katika makala yangu ya mwanzo, kugombana na madaktari si jambo jema. Nilikumbushia usemi wa wahenga kuwa tusidharau wakunga na uzazi ungalipo. Napenda kuongezea kwa dhati kabisa kuwa kugombana na madaktari si dalili njema bali ni uchuro.

Wednesday, 27 June 2012

KIONGOZI WA MADAKTARI ATEKWA, AOKOTWA AKIWA KATIKA HALI MBAYA

Dk. Steven Ulimboka.
Taarifa zilizotufikia ni kwamba Kiongozi wa Mgomo wa Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka ametekwa na ameokotwa akiwa katika hali mbaya sana.

Kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forums, Dk Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye 'face to face' kwa ajili ya mazungumzo.

Tukio hilo limetokea wakati kumekuwepo na mgomo wa madaktari nchi nzima ambao hata hivyo wameonekana kusalitiana kwa kutokuwa na msimamo wa pamoja, kwani maeneo mengine huduma zimeendelea kama kawaida.

UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka:

Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.
---
UPDATE:

Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------

Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.

Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza kuzungumza.

Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka.

Tuesday, 26 June 2012

Tume ya Mabadiliko ya Katiba yatoa ratiba ya kazi ya kukusanya maoni

 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilo ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatarajia kuanza kufanya mikutano na wananchi wa mikoa minane kuanzia siku ya Jumatatu, Julai 2, 2012 hadi Jumatatu, Julai 30, 2012 kwa lengo la kukusanya maoni yao kuhusu Katiba Mpya
 
Mikoa hiyo ni Dodoma, Kagera, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Manyara, Pwani, Shinyanga na Tanga. Katika mkoa wa Dodoma, Tume itaanza na Wilaya ya Bahi; Katika mkoa wa Kagera Tume itaanza na wilaya ya Biharamulo; Katika mkoa wa Manyara Tume itaanza na wilaya ya Mbulu na katika mkoa wa Pwani Tume itaanza na wilaya ya Mafia.
 
Kwa mkoa wa Shinyanga Tume itaanza na wilaya ya Kahama na kwa mkoa wa Tanga, Tume itaanza na Wilaya ya Lushoto. Kwa Zanzibar, Tume itaanza kukusanya maoni katika mkoa wa Kusini Unguja katika wilaya ya Kusini.
 
Taratibu zote za kuanza kazi zimekamilika zikiwemo kuandaa ratiba na kuisambaza katika mikoa na wilaya husika. Wajumbe wa Tume na watumishi wa Sekretarieti wamejigawa katika makundi saba. Kila kundi litafanya mikutano katika mkoa mmoja isipokuwa kundi moja litakalofanya mikutano katika mikoa miwili ya Kusini Unguja na Kusini pemba.
 
Tume inawaomba wananchi kuhudhuria mikutano itakayoitishwa na Tume na kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yao kwa uwazi, uhuru na utulivu.
 
Pamoja na kuwasilisha maoni kupitia mikutano itakayoitishwa na Tume, wananchi pia wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia tovuti ya Tume (www.katiba.go.tz) au kwa njia ya posta kupitia anuani za zifuatazo:                     
i.   Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Makao Makuu, Mtaa wa Ohio, S.L.P 1681, DAR ES SALAAM, Simu: +255 22 2133425, Nukushi: +255 22 2133442; 
 
Au
 
ii.   Jengo la Ofisi ya Mfuko wa Barabara, Mtaa wa Kikwajuni Gofu, S.L.P. 2775, Zanzibar, Simu: +255 224 2230768, Nukushi: +255 224 2230769

Mahakama kuu ya Tanzania Kitengo cha kazi leo kimetoa onyo kwa Chama cha Madaktari Nchini (MAT) kuzingatia amri ya Mahakama hiyo iliyotolewa siku ya Ijumaa tarehe 22 Juni 2012 ya kusitisha na kutoshiriki katika mgomo na kumtaka Rais wa Chama cha Madaktari kutangaza kutii amri hiyo kupitia vyombo vya habari.


Twiga Bancorp yashinda tuzo ya Dhahabu ya Utoaji Huduma bora duniani

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo (kulia) akipokea Tuzo ya utoaji bora wa huduma  ijulikanayo kama ‘Century International Gold Quality ERA Award’, kutoka kwa Rais na Afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya Kimataifa ya Business Initiative Directions, Jose Priento mjini Geneva-Uswisi. Twiga Bancorp imepata tuzo hiyo,kwa utoaji huduma zinazoridhisha kwa wateja, Uongozi bora, Mipango mkakati inayokidhi haja ya wateja  kama inavyotambulika katika QC 100 TQM.
Hivi karibuni Benki hiyo ilitunukiwa Tuzo ya Dhahabu iliyotolewa na jijini Geneva Uswis, tuzo hiyo inajulikana kama Century International Gold Award (ERA).

Lengo la tuzo hiyo ni kutambua ubora wa huduma zitolewazo kwa wananchi na taassisi au kampuni mbalimbali lengo lokiwa ni kuhamasisha utolewaji wa huduma bora kwa wateja.

Mtendaji Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Hussein Mbululo amesema  kwamba Benki yake ilikuwa miongoni mwa Benki 100 zilizoshinda katika tuzo hizo kutoka nchi 47, tuzo hizo ziligawanywa katika makundi saba.

Amesema kujituma miongoni mwa wafanyakazi katika kuwahudumia wateja pamoja na ubunifu ndio siri kubwa ya mafanikio. 

Twiga Bancorp ni Benki inayo milikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%).  
Afisa Mtendaji wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akiwa na baadhi ya maofisa wa BID mjini geneva kabla ya kuanza utoaji Tuzo.  
CEO wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akisalimiana na Rais na CEO wa BID, Jose Priento mjini Geneva-Uswisi

Monday, 25 June 2012

KESHO TAREHE 26 MWEZI WA SITA NI KUMBUKUMBU YA AMINA CHIFUPA




Ilikuwa tarehe 26 mwezi wa sita tulimpoteza Mh: Amina Chifupa .Ikiwa pia ni siku ya upigaji vita wa madawa ya kulevya nchin Tanzania
Mh: Amina chifupa ametimiza miaka mitano toka alipo fariki tuta endelea kumuenzi kwa ucheshi wake mmungu amuweke panapo stahiki
 Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa mbunge wa viti maalum wa chama cha mapinduzi CCM

Sunday, 24 June 2012

Saturday, 23 June 2012

Kampeni ya Kubandika Stika Zenye Namba za Simu za Vituo Mbalimbali za vituo Vya Polisi Yazinduliwa Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi  akibandika stika hizo.
 Kamanda Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua kampeni ya kubandika stika zenye namba za simu za vituo mbalimbali ambazo abiria watazitumia kwaajili ya kutoa taarifa za usalama na matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani. Kampeni hiyo inadhaminiwa na benki ya posta (TPB)

IKULU:Rais Jakaya Kikwete Akiifariji Familia ya Aliyekuwa Mkuu wa Utawala CCM Makao Makao Makuu Dodoma Marehemu Mwangunza Kinyamagoha

 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Mkuu wa Utawala CCM Makao Makao Makuu Dodoma marehemu Mwangunza  Kinyamagoha nyumbani kwake mjini Dodoma jana.Marehemu Kinyamagoha alifariki hivi karibuni. 



 Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Kinyamagoha nyumbani kwake mjini Dodoma jana kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.Picha na Freddy Maro-IKULU

AWATAKA MADAKTARI KUSITISHA MGOMO WAO

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari  ofisini kwake kuhusu mapokezi ya Mwenge wa Uhuru utakaowasili jijini Dar es Salaam wiki ijayo ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba. Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa wanananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge huo.

Na. Adrophina Ndyeikiza na Aron Msigwa – Ofisi ya RC -DSM
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru utakaowasili  jijini Dar es salaam siku ya jumatatu ukitokea mkoa wa Kusini Pemba.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema kuwa Mwenge wa Uhuru utakabidhiwwa kwa uongozi wa wilaya ya Temeke saa 4 asubuhi na kuanza mbio zake ukipita katika wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam kwa muda wa siku 3.
 
Amesema mbio za Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu zinaongozwa na Kauli Mbiu ya Shiriki Kikamilifu Katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi na Mapambano dhidi ya Rushwa, Ukimwi na Dawa za kulevya.
 
Ameto wito kwa waajiri na wakuu wa taasisi zote za Serikali kushiriki kikamilifu katika maeneo yao ya kazi kuulaki Mwenge huo.
 
Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametoa msimamo wa mkoa wa Dar es salaam kuhusu mgomo wa madaktari kwa kuwataka madaktari hao kusitisha mgomo wao na kutoa huduma kwa wananchi kama kawaida.
 
Amesema kufuatia Chama cha Madaktari nchini  (MAT) kutangaza kuanza  mgomo wa madaktari nchi nzima mkoa wa Dar es Salaam umefuatilia kwa karibu mgomo huo na kubaini kuwa hospitali zote za Serikali za mkoa huo zimeendelea kutoa huduma kwa wananchi kama kawaida.
 
Bw. Meck  Sadiki ameeleza kuwa hakuna taarifa zozote za kugoma kwa  madaktari waliopangiwa zamu katika hospitali za Mwananyamala, Kinondoni na Temeke na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
“ Ninachukua fursa hii kuwapongeza madaktari wote wa hospitali za Serikkali za mkoa wa Dar es salaam waliooendelea kutoa huduma kama kawaida licha kutangazwa kwa mgomo kwa kuonyesha nia ya kugoma na kutii sheria”. Amesema.
 
Amewataka wale wote wanaoendesha mikutano ya kuhamasisha migomo ndani ya maeneo ya hospitali za serikali kuacha mara moja huku akisisitiza kuwa serikali haitawavumilia na watakaobainika watachuliwa hatua za kisheria.
 
“ Ninatoa angalizo kwa wale wote wanaopenyeza mikutano ndani ya maeneo ya hospitali za serikali waache mara moja kwa sababu majengo yale ni kwa ajili ya matumizi ya huduma za afya tu”
 
Ameongeza kuwa tayari suala la mgomo wa madaktari liko katika vyombo vya sheria na kufafanua kuwa tayari mahakama ya kazi imeshabainisha wazi kuwa mgomo wa madaktari ni batili.
 
“ Kwa bahati nzuri suala hili limepata nguvu kisheria kwa kuwa mahakama imeshabainisha wazi kuwa mgomo wa madaktari hao kuwa  ni batili na kwa yeyote yule atakekutwa ndani ya maeneo ya hospitali akiendesha mikutano sheria itafuata mkondo wake” amesema.
 
Aidha mkuu wa mkoa huyo amebainisha kuwa maeneo yote ya hospitali ni maeneo ya kutolea huduma za afya kwa wananchi na si mahala pa kuhamasisha mikutano ya kisiasa na kutoa onyo kwa vikundi vyote vinavyojiita vikundi vya wanaharakati kutopenyeza harakati zao katika maeneo hayo

Friday, 22 June 2012

Mbowe, Lissu, Mdee wamzima Ngeleja



MAKEKE ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (CCM), jana yalizimwa na wabunge watatu wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Halima Mdee, huku wakimtaka Spika wa Bunge amchukulie hatua kwa kupoteza muda.
Ngeleja aliyekuwa akichangia hotuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2012/2013 muda mfupi baada ya Mbowe, alitumia muda mwingi kuishambulia hotuba ya maoni ya bajeti ya Kambi ya Upinzani akidai ni mbovu na haitekelezeki.
Huku akishangiliwa na wabunge wenzake wa CCM, Ngeleja ambaye pia ni Mbunge wa Sengerema, alikwenda mbali zaidi akinuku hotuba hiyo iliyowasilishwa na Waziri kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, na kusema kuwa wana vyanzo vya ukusanyaji mapato ambavyo vinaonesha shilingi sifuri.
Kama hiyo haitoshi, mbunge huyo aliitaka Kambi ya Upinzani kuwaomba radhi Watanzania akidai wamewapotosha kutokana na kuandaa bajeti iliyowahadaa wakati wameshindwa kuainisha uwiano wa vyanzo vya mapato na matumizi.
Hatua hiyo, ilimfanya mnadhimu mkuu wa kambi hiyo, Lissu kusimama na kuomba mwongozo wa Spika akisema kuwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge, bajeti iliyoko mbele yao ambayo inapaswa kujadiliwa ni ile iliyowasilishwa na serikali.
“Sisi wapinzani tunawasilisha maoni yetu kuhusu bajeti ya serikali ili yafanyiwe kazi na si bajeti kivuli wala mbadala kama baadhi ya wabunge wanavyojaribu kupotosha,” alisema Lissu na kuungwa mkono na Spika.
Spika Anne Makinda alifafanua kuwa hakuna bajeti kivuli wala mbadala na badala yake kambi hiyo hutoa hoja ya kuhusu bajeti ya serikali inayokuwa imesomwa ikionesha kama wao wangekuwa madarakani wangeipanga hivyo.
Hata hivyo Ngeleja aliikataa taarifa hiyo na hivyo kuzidi kushikilia msimamo wake, jambo lililomlazimu Mbowe, kuomba mwongo wa Spika akiuliza kiti chake kinawachukulia hatua gani wabunge kama hao wanaopoteza muda kwa jambo lililokwisha kufafanuliwa.
Wakati Spika akijaribu kumaliza ubishi huo, Mbunge wa Kawe, Mdee, aliinuka na kuomba kumpa taarifa Ngeleja na kusema kuwa kipengele anachokisemea mbunge mwenzake kilishatolewa ufafanuzi kwamba kulikuwa na kasoro za uchapaji.
“Huyu ana uchungu wa kutemwa katika Baraza la Mawaziri,” alisema Mdee lakini kabla ya kuendelea Spika alimtaka afute maneno hayo kwanza.
Mdee alidai kuwa hatua hiyo inaonesha ni jinsi gani Ngeleja haudhurii vikao, kwani asingepoteza muda kuhoji jambo ambalo walikwisha kulifanyia masahihisho.
Awali wakati wa mchango wake, Ngeleja alisema kuwa hali ya uchumi wa nchi yetu kwa sasa inachangiwa na upungufu wa chakula ambapo bei ya bidhaa hiyo imepaa na kuongeza makali ya maisha kwa wananchi.
Ngeleja alisema pia tatizo la nishati limekuwa chanzo cha kuongeza makali ya maisha kwani bei ya nishati imekuwa ikipaa mara kwa mara.
Naye Mbowe katika mchango wake, mbali na kulalamikia deni la taifa na kuitaka serikali ifanye juhudi za makusudi kuwaondoa wananchi kwenye umaskini walionao sasa, pia alikemea lugha za matusi kwa baadhi ya wabunge, hivyo kumtaka spika na wasaidizi wake kutenda haki kwa pande zote.
Shellukindo awasifu wapinzani
Akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo, (CCM), alianza kwa kuipongeza kambi ya upinzani bungeni akisema kuwa inafanya kazi yake vizuri kwa kuishauri na kuikosoa serikali.
Shellukindo aliwataka wabunge wenzake wa chama tawala kuweka mambo ya vyama pembeni na kuangalia masilahi ya taifa, kwani kazi ya wabunge wote bila kujali itikadi za vyama ni kuishauri serikali katika masuala ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema hakuna Bunge katika nchi yoyote ambalo ni la chama tawala wala cha upinzani, huku akiwapongeza wapinzani kuwa wanakitakia mema CCM kwa kuwakosoa ili warekebishe.
Aidha, mbunge huyo alikosoa sera ya Kilimo Kwanza huku akibainisha kuwa haimlengi mkulima wa kawaida bali ni wakulima wakubwa.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Selukamba (CCM), alisema mfumuko wa bei unachangiwa na ubovu wa miundombinu jambo ambalo husababisha mazao yanayotoka shambani ambako ni vijijini kufika mjini na kuwa katika bei ya juu kuliko yalivyozalishwa.
Selukamba alibainisha kuwa mazao au bidhaa ikitoka kijijini inapofika mjini huuzwa kwa bei ya juu zaidi kutokana na gharama kubwa kutumika katika usafirishaji wake.
Filikunjombe aigomea bajeti
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), naye amekuwa kama mwenzake wa Kisesa, Luhaga Mpina, kwa kugoma kuiunga mkono bajeti ya serikali akitaka maelezo ya serikali kuhusu fedha za miradi ya maendeleo zilizotengwa katika Wizara ya Uchukuzi.
“Katika bajeti iliyopita tulisema na serikali kupitia waziri mkuu, ikatangaza kuongeza sh bilioni 90 kwa Wizara ya Uchukuzi na kati ya hizo sh bilioni sita, zilipelekwa katika sekta ya meli Ziwa Nyasa na fedha zilizoletwa ni sh milioni 200 pekee,” alisema.
“Nawaomba wabunge wenzangu tuwe wakweli, kwa hili  lazima tuihoji, na kwa serikali hii ya CCM ni yetu, kama hatutafanya hivyo tutakuwa hatuna maana ya kuwapo kwetu hapa bungeni,” alisema Filikunjombe.
Mkono aibua ufisadi
Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, ameibua ufisadi unaodaiwa kufanywa katika mgodi wa Kiwira na kulitaka Bunge kuunda kamati maalumu ya uchunguzi.
Mkono alidai kuwa sehemu moja ya mgodi huo yenye utajiri mkubwa imeuzwa kwa bei ya kutupwa kwa kampuni moja ya Australia.
Alisema uuzaji huo ni kinyume cha makubaliano yaliyofikiwa na Bunge  mwaka 2007 ambapo liliagiza kuwa mgodi wa Kiwira uliokuwa umeuzwa kwa Kampuni ya Tan Power urudishwe serikalini baada ya kuwa umeuzwa kwa dola laki saba tu.
Hata hivyo, Mkono alisema kuwa katika hali ya kushangaza Kampuni ya Tan Power ambayo ilikuwa imeingia ubia na serikali iliuzwa kwa Waustralia  kiasi cha mabilioni ya dola.
“Mheshimiwa Spika, Kiwira kulikoni? Lini Bunge litaunda kamati ya kwenda kuangalia Kiwira?” alihoji na kusema kuwa pamoja na yote hayo, sasa serikali imetenga sh bilioni 40 kwa ajili ya mradi wa Kiwira na kuhoji nani aliteketeza fedha za awali zilizotolewa kwa ajili hiyo.

Tanzania yajiandaa kufufua mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa


Tanzania inajiandaa kurejesha mpango wa taifa wa jeshi la Kujenga Taifa, ambao ulisitishwa miaka 20 iliyopita, kufuatia wito wa kufufuliwa kwa shughuli hizo kama chombo cha mshikamano wa kijamii.
Vikosi vya ulinzi vya jeshi la Tanzania wakicheza gwaride Dar es Salaam. Serikali ilitenga pesa katika bajeti ijayo ili kurejesha mpango wa taifa wa Jeshi la Kujenga Taifa. [Na Mwanzo Milinga/AFP]
Mpango huo ni mafunzo ya kijeshi ya mwaka mmoja ambapo Watanzania watatakiwa kushiriki kabla ya kujiunga na taasisi za elimu ya juu.
Mpango wa jeshi la Kujenga Taifa ulianzishwa mwaka 1963 na rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere. Ulisitishwa mwaka 1994 baada ya ukosefu wa fedha.
Pamoja na mafunzo ya kijeshi yenye kiwango, mpango huu pia hutoa mafunzo juu ya haki za binadamu, elimu ya uraia, na historia ya Tanganyika na zanzibar, na pia unakusudiwa kuamsha hisia za umoja na uzalendo kwa wanafunzi.
Waziri wa Fedha wa Tanzania William Mgimwa aliliambia bunge wiki iliyopita kuwa kisasi cha shilingi bilioni 7.5 (dola milioni 4.7) zitatengwa katika bajeti ijayo ili kufufua mpango wa Jeshi la Kujenga Taifa.Kwa kuanzia, wanafunzi 5,000 tu wahitimu wa elimu ya juu watachaguliwa kushiriki katika mpango huo.
Makala zinazohusiana

Thursday, 21 June 2012

MAAJABU: WANAIJERIA HUUZA FIGO KWA SH MILION 51($30,000)

Baadhi ya wanaijeria waishio nje ya nchi wamejikuta wakiwa na maisha magumu kiasi cha kuamua kuuza figo zao ili waweze kuishi.
Biashara hiyo iliyoshamiri kwenye mtandao imewafanya baadhi yao kutafuta soko la viungo hivyo muhimu kwenye mwili wa binadamu na wengine wakisafiri hadi Malaysia na India kuuza figo zao zote mbili kwa $30,000.
Kwa mujibu wa mtandao wa nigeriafilms.com, watafiti wake wamebaini kuwa kuna mtandao mkubwa sana wa wafanyabiashara, mawakala, wauzaji wa watafutaji wa bidhaa hiyo ambao hutafuta watu watakaouza figo zao.Wengine hufikia hatua za kuteka watu na kuwanyofoa figo zao ili kujipatia maisha mazuri na ya haraka.Kuna taarifa kuwa watu wengine hupoteza maisha wakati wa oparesheni ya kunyofoa figo hizo.Mpaka sasa karibu wanaijeria 1000 wana matumaini ya kupata connection hizo ili nao waweze kuuza figo zao na kujipatia maisha wanayoyataka.Mtandao huo umemaliza kwa kusema, “Hivi ndivyo umaskini unaosababishwa na uongozi mbovu umeifikisha Nigeria.”

Sunday, 10 June 2012

MAMLAKA YA MAJI ARUSHA YALALAMIKIA HUJUMA



MAMLAKA ya maji safi na maji taka Jijini Arusha(AUWSA ),imebaini kuhujumiwa wa watu mbalimbali wakishirikiana na wafanyakazi wake, wasio waaminifu kwa kuunganisha maji kinyume cha utaratibu na kusababisha upotevu mkubwa wa  mapato.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa AUWSA, Eng.Ruth Koya alisema jana kuwa, tayari wamefanikiwa kuwanasa wezi wa maji zaidi ya 100 waliojiunganishia  kinyume  na utaratibu,  wakiwemo vigogo  wa halimashauri ya Arusha,ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo kwa kipindi kirefu,bila kulipa chochote na kuisababishia hasara kubwa mamlaka hiyo.

Vigogo wa halmashauri waliokamatwa ni pamoja na Afisa mali asili, mazingira na ardhi, Maico Myairwa ambaye yeye aling’oa  kabisa mita ya idara ya maji, ambayo imekutwa chumbani mwake, ameificha huku akijua ni kosa kisheria.

Mwingine ni fundi mkuu wa maji wa halmashauri ya Arusha,Loishono Mollel ambaye  amejiunganishia maji  baada ya kutoboa bomba kubwa la idara ya maji na kupitisha mpira mrefu kwa chini, hadi nyumbani kwake ambapo pia alikuwa akiyatumia maji hayo kustawisha  bustani yake.

Hata hivyo Mollel amebainika kuwa  kinara mwenye mradi wa kuwaunganishia maji watu mbalimbali kinyemela, huku wakimlipa kiasi kikubwa cha fedha ,ambapo mamlaka hiyo imengóa mtandao wa mabomba yote aliyoyaunganisha kwa wakazi mbalimbali eneo la Sekei na kufanya familia zaidi ya 20, kukumbwa na adha ya kukosa maji.

Pia meneja  wa maji wa halmashauri ya Arusha, Criston Kimaro ambaye ndiye anadaiwa kutoa idhini ya watu kuunganishiwa maji bila kufuata utaratibu huku watu hao wakimlipa fedha ya kuwaunganishia pamoja na malipo ya mwezi katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.

Operesheni hiyo ikiongozwa na mkurugenzi wa maji safi na maji taka wa jiji la Arusha ,Engineer  Koya na kuambatana na maafisa wengine ,imekuja kufuatia kuwepo taarifa za upotevu mkubwa  wa maji, tofauti na kiwango kinachozalishwa kwa siku na kufanya idadi kubwa ya wateja wake, kutopata huduma ya maji safi baada ya nusu ya maji yanayozalishwa, kuishia njiani kwa wajanja wachache.

Eng,Koya alisema  maji yanayozalishwa na AUWSA ni mengi kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali, lakini amekuwa akishangazwa kupata malalamiko ya kila mara kutoka kwa wateja wake wa kudumu na wapya kwamba hawapati huduma hiyo.

Alisema Operesheni hiyo ni yakudumu lengo ni kuhakikisha wanaondoa mtandao wa wezi wa maji, ambao wamekuwa wakijinufaisha bila kuilipa chochote mamlaka hiyo,na kwamba  watawafikisha mahakamani watu wote waliohusika na wizi huo wa maji iwapo watashindwa kulipa fidia katika kiwango walichotumia .

Naye mkuu wa kikosi cha operesheni wa AUWSA,Mohamed Isumail alisema, tangu kuanza kwa zoezi hilo,Mei 29 mwaka huu watu zaidi ya 100 kutoka maeneo ya Moshono,Sekei,Lemara  na Ungalimited wamekamatwa, baada ya kubaini  wamejiunganishia  huduma ya maji na kutumia kinyume na utaratibu .

Aidha alisema maeneo yaliyokithiri kwa wizi wa maji jijini hapa ni ,Sekei,Moshono Migungani na Baraa, ambapo idadi kubwa ya wakazi wa maeneo hayo, wanaiba maji baada ya kuunganisha mipira mirefu chini ya Ardhi huku wakiwahadhaa waofisa wa maji waporika, kuwa maji wanayotumia yanatoka kwenye bomba la kijiji ambayo mara nyingi hayalipiwi.

Isumaili ambaye pia ni kaimu Mhandisi,uendeshaji na matengenezo AUWSA,aliongeza kuwa changamoto kubwa wanayoipata katika zoezi hilo, ni pamoja na watu kujifungia ndani na kugoma kutoa ushirikiano wakati wa zoezi hilo.


Thursday, 7 June 2012

EURO 2012: ITALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI YA WENDAWAZIMU CASSANO NA BALOTELLI

Maneno ya Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania.
Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kujenga ukuta wa chuma na kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza kwa ajili ya mfumo ambao unatumia na Spain, ambao mpaka sasa umeleta matokeo ya mchanganyiko. italy haikufungwa hata mechi moja kwenye hatua ya kufuzu, lakini wamekuwa wakifungwa kwenye mechi za kirafiki. Skendo ya upangaji wa matokeo ambayo inaliandama soka la nchi hiyo kwa miaka mingi sasa, haitegemewi kuwa na madhara makubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa katika miaka 1982 na 2006, sababu kubwa ni kwa kuwa ni wachezaji wachache wa kikosi cha sasa wameguswa na kashfa hiyo, lakini suala hilo bado linabakia kuwa sio zuri kwa wachezaji.
Droo ya group C haikuwa nzuri kwa Italy, lakini atleast mechi yao dhidi ya Spain itakuwa ya kwanza. Na kupata pointi kutoka kwenye mechi hiyo ni jambo ambalo linawezekana, kwa kuangalia Spain huwa na kawaida ya kuanza vibaya michuano mikubwa, ukiangalia kombe la dunia lilopita walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza makundi. Baada ya mechi hiyo atleast kidogo mambo yanaweza kuwa mazuri dhidi ya Croatia na Ireland.

KARIBU