..

..
.

Wednesday, 31 December 2014

COASTAL WATOA SARE NA TANZANIA PRISON

466559_heroa
Coastal union ya jijini Tanga wametoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa sokoine.

Katika mchezo huo wa leo uliotanguliwa na mvua na kupelekea uwanja kuwa na utelezi kila upande wametengeneza nafasi ambazo hakuna aliyeitumia vyema.

Katika hatua nyingine mchezo wa ligi kuu ya vodacom kati ya mtibwa sugar na stand united ulivunjika katika dakika ya 6 kama tulivyo ripoti hapo awali na mchezo huo unatarajiwa kuhitimishwa kesho saa mbili asubuhi.

Friday, 26 December 2014

HIZI NDIZO MBWEMBWE ZA KRISMASS TANGA JANA

  Wakazi wa Tanga na vitongoji vyake wakisherehekea Sikukuu ya Krismass  katika ufukwe wa Bahari ya Hindi beach ya Raskazone jana





Saturday, 22 February 2014

Coastal Union Vs Mbeya City

 Dany, Selembe na Santo wakimsikiliza mwalimu kwa umakini leo asubuhi katika kambi ya Coastal Union.

                                Kocha Yusuf Chipo akisisitiza jambo kabla ya mechi leo asubuhi.

                      Mtu mzima Boban, akitafakari namna atakavyowanyamazisha Wanyakyusa.


                                  " Lazima mucheze kwa kujiamini tupo nyumbani baanaaa.."

Kocha wa magolikipa Adam Meja na kocha msaidizi Ally jangalu wakifuatilia darasa la Mwalimu Chipo.



KOCHA wa Coastal Union, Yusuf Chipo amesema mechi ya leo ni ngumu haina matokeo lakini watakaoleta matokeo ni wachezaji baada ya kuamua kucheza kwa kujituma.
Chipo, ameongeza kuwa amesikia Mbeya City ni timu ngumu, lakini yeye hajui hilo kwasababu alipokuwa darasani akifundishwa ukocha ncini ujerumani, aliambiwa timu zote zinakuwa na wachezaji kumi ndani na golikipa mmoja.
“Sitegemei kuona kitu kipya kutoka kwa Mbeya City, bali nataka kuwaona nyinyi mnacheza kitimu na kujituma, sitaki mtu akae nyuma pelekeni timu mbele sisi tupo nyumbani tunataka ushindi. Kinachowasaidia Mbeya City kupata sifa ni kujituma, na hicho naamini hata nyinyi mnaweza,” alisema.
Baada ya hapo alitaja kikosi cha leo na kuwaambia macho ya mashabiki wa Coastal Union, kwenye mchezo huu wa Ligi Kuu Tanzania bara yapo miguuni mwenu, mkifanya vizuri ama mkifanya vibaya ni kwa mustakabali wa maisha yenu kisoka.
Kikosi cha leo kitakachoanza: Shaaban Kado, Mbwana Kibacha, Abdi Banda, Yusuf Chuma, Juma Nyoso, Jery Santo, Danny Lyanga, Ally Nassor ‘Ufudu’, Ayoub Semtawa, Crispian Odula na Haruna Moshi ‘Boban’.
Wachezaji wa akiba: Mansour Alawi, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Yayo kato, Mohammed Miraji, Ayoub Masoud, Behewa Sembwana na Kenneth Masumbuko.
Coastal Union inashuka dimbani kumenyana na Mbeya City, wakiwa na point 22 nafasi ya saba katika msimamo wa ligi, ushindi wa leo dhidi ya Mbeya City utamaanisha vitu viwili, kupata uhakika wa kumaliza ligi nafasi nzuri na kuweka heshima kwa kuwafunga Mbeya City wanaotajwa kuwa wagumu kufungika.
HAFIDH KIDO
MSEMAJI CUSC
TANGA- TANZANIA
FEB 22, 2014

Saturday, 11 January 2014

COSTAL UNION KUWASILI NCHIN OMAN KWA AJILI YA KUJIPANGA ZAID NA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI YA VODACOM




















TIMU ya Coastal Union jana iliwasili jijini Muscat Oman usiku saa sita na kufikia katika hoteli ya City Centre.
Kaimu balozi wa Tanzania nchini Oman, ndie alietupokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mascut na kutuelekeza vema kuhusu masual mazima ya mji huo.
Nae mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Talib Hilal alikuja hotelini na kuzungumza nasi juu ya masuala mazima ya soka nchini hapa.
Talib, ndie mwenyeji wetu ambae anaratibu kila tukio tutakalofanya kuhusu mechi na mazoezi ya timu. Vilevile atahakikisha maisha yetu mjini Mascut yanakuwa rahisi kwa kusimamia masuala ya usafiri na mambo yote muhimu.
Kesho saa tisa alasiri timu itashuka dimbani katika uwanja wa Musanaa ambapo tutacheza mechi ya kirafiki na timu ya Musanaa ambayo ipo ‘top four’ ya ligi kuu ya Oman.
Aidha zipo taarifa zilizotolewa na moja ya gazeti la udaku juu ya hali mbaya ya maisha kwa timu ya Coastal Union, nchini Oman. Lakini nadhani picha zinazungumza maneno mengi kuliko maandishi. Hivyo kwa nafasi ya usemaji nahakikisha kuwa vijana wapo katika hali nzuri na hakuna matatizo yoyote.
Kwa mujibu wa mkuu wa msafara ambae pia ni mwenyekiti wa Wagosi, Hemed Hilal ‘Aurora’ timu itacheza mechi nne za majaribio kabla ya kurudi Tanzania baada ya wiki mbili.
Taarifa nyingine zitaendelea kutolewa kupitia vyanzo vyote vya Coastal Union……
COASTAL UNION
MUSCAT, OMAN
10 JANUARI, 2014

Saturday, 4 January 2014

KIKOSI CHA COASTAL UNION CHA KAMILIKA KWA WACHEZAJI WOTE KUWEPO MAZOEZINI

Jana nilizungumza na mwalimu Chippo, amefurahishwa na vijana namna wanavyopiga mazoezi kwa kujituma na kufanya kila wanachofundishwa kwa usahihi...... Una maoni? Kwa walio Tanga hebu tupeni tathmini ya mazoezi ya vijana wetu.

Sunday, 15 December 2013

BREAKING NEWS : Mwenyekiti wa CCM Mwanza CLEMENT MABINA auwawa na wananchi wenye hasira kali.

Breaking News: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza (Mabina) auwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe

Taarifa zaidi, soma hapa => http://bit.ly/18O5nYu
 Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndg CLEMENT MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini Mwanza
Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani? Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewan
Risasi zilipomuishia na kufanikiwa kumuua raia m1 kwa risasi ndipo wananchi wenye hasira kali wakamrudia kumpiga wakiwa na mapanga, mawe na kila dhana ya kijadi, jambo lililopelekea umauti kumkuta. Mauaji yametokea mchana huu majira ya saa 7.


KARIBU