..

..
.

Friday, 17 August 2012

TANGA ALL STARS WAMTOSA ZITTO KABWE.


Habari za kuamika kutoka kwa vyanzo mbalimbali zinadai kuwa wasanii wa mkoa wa Tanga wamelikataa wazo la mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe la kufanya wimbo wa pamoja kama Tanga All Stars kwa madai kuwa mradi huo anaufanya ili kujinufaisha kisiasa.

Hivi karibuni Mheshimiwa Zitto alikiri kuutaka urais wa Tanzania wakati wa mahojiano na kipindi cha Makutano cha Magic FM na watu wengi wamekichukulia kitendo cha kuwa karibu na wasanii wa Tanzania kama njia ya ya kujiimarisha kisiasa na kuwashawishi vijana walio wengi nchini.

  Mwandishi wetu ameongea na MwanaFA kwa simu jana (August 17) ambaye amesema wasanii wa Tanga wana program yao wenyewe iliyopo tangu muda mrefu na wamewahi hata kufanya show za ndani na nje.

Amesema hawawezi kujiingiza kwenye mradi huo wa Zitto kwakuwa umekaa kisiasa zaidi.

Katika mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM mwezi uliopita, Zitto alidai kuwa lengo lake ni kila mkoa kuwa na wimbo wa nyota wenye asili ya mikoa mbalimbali na baada ya Kigoma mkoa wa pili aliokuwa anafanya nao mazungumzo ni Tanga ambao tayari wamemtosa.

Wakati Tanga ikishtukia mchezo huo wenye harufu ya siasa, wasanii wa Morogoro chini ya Afande Sele tayari wameingia mkenge na wamefanya wimbo wa Morogoro All Stars.

Morogoro All Stars inaundwa na Afande Sele, Koba, Stamina, Belle9, Samir, Criss Wamaria, Nassa, Oten, Dayna na Zilla!

KEKO ATAPIGA SHOW KALI JIJINI MWANZA WEEKEND HII


Rapper wa kike wa nchini Uganda Keko anatarajiwa kupiga show weekend hii jijini Mwanza.

KARIBU