Pages

Thursday, 6 September 2012

Jumuiya za habari Tanzania vyataka uchunguzi kwa kifo cha mwandishi wa habari

Jukwaa la Wahariri nchini Tanzania (TEF) na Baraza la Habari la Tanzania (MCT) wametaka uchunguzi huru kwa kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, liliripoti gazeti la The Citizen la nchi hiyo hapo Jumanne (tarehe 4 Septemba).
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, aliliambia gazeti la Daily News la Tanzania kwamba ataongoza uchunguzi wa tukio hilo. TEF na MCT wamekubali kuchangia kwenye uchunguzi huru
Makala zinazohusiana 

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATANGAZA KUKIFUTIA USAJIRI CHAMA CHOCHOTE KITAKACHOKIUKA SHERIA ZA NCHI


Kutokana na kuendelea kwa mfululizo wa matukio mbalimbali yanayosababishwa na vurugu za kisiasa kati ya baadhi ya vyama vya siasa dhidi ya jeshi la polisi, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Tanzania imesema imechoshwa na matukio hayo ambayo yamekua yakisababisha vifo vya mara kwa mara kwa raia wasio na hatia.

Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa amesema ofisi yake kuanzia sasa imepanga kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo kukifuta chama chochote cha siasa kitakachothibitika kufanya mkutano kinyume cha sheria na kusababisha vurugu pasipo kujali kama vurugu hizo zimedhuru au hazijadhuru raia yeyote.

Vilevile Tendwa amekemea kampeni mbalimbali zinazoendelea kufanywa nchi nzima na baadhi ya vyama vya siasa na kupewa jina la ‘OPARESHENI’ ambapo amedai kuwa huu si wakati wa vyama kuanza kampeni, hivyo chama chochote kitakachoendelea na kampeni kwa mtindo huo kuanzia sasa kitachukuliwa hatua kali ikiwemo kukifutia usajili.

LIPUMBA AZUNGUMZIA KUSAJILIWA KWA CHAMA ADC NA KUHAMA KWA BAADH YA VIONGOZI WA WA CHAMA CHA CUF

  Chama cha CUF Tanzania kimesema kupatiwa usajili wa kudumu kwa chama kipya cha ADC ambacho wanachama na viongozi ni wale waliotoka chama hicho cha CUF hakumaanishi ushawishi wa chama hicho sasa umefika mwisho wake.
Akizungumzia kusajiliwa kwa chama hicho mwenyekiti wachama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba hata hivyo ametilia wasiwasi namnachama hicho kilivyopata usajili wa kudumu tofauti na inavyokuwa kwavyama vingine vya siasa.
Na suleiman KIBUGA